Zuchu Amvuta Shati Kiba





MUZIKI wa sasa ni ushindani. Unaambiwa licha ya AliKiba kutangulia kuachia ngoma yake ya Ndombolo, mrembo kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Zuchu ameibuka na kuachia ngoma yake iitwayo Nyumba Ndogo ambayo inaonekana kumkaba koo mkongwe huyo.

Awali, Kiba ndiye aliyetangulia kuachia audio ya wimbo wake wa Ndombolo Juni 10, mwaka huu na mpaka sasa wimbo huo una views 647,385 lakini Zuchu akaibuka Juni 15 na Nyumba Ndogo ambayo tayari ina wafuasi 356,865.


Kiba alipoona mtoto wa kike anakuja kwa kasi, Juni 15 hiyo hiyo naye akaachia video ya wimbo huo wa Ndombolo lakini hata hivyo, video hiyo ni kama inakwenda sawa na audio ya Zuchu kwani Ndombolo (video) ina views 367,422 huku Nyumba Ndogo (audio) ikiwa na 357,797.

Hii inatoa picha gani? Kama Zuchu ataachia video sasa hivi, ni dhahiri anaweza kumfikia Kiba kama si kumpita kabisa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad