Aliyetaka kuzamia Olimpiki Japan aachiwa huru




Polisi nchini Uganda wamemuachia mwanamichezo mnyanyua vitu vizito aliyerudishwa nchin humo kutoka Japan juma lililopita baada ya kutoweka.



Muda mfupi baada ya kuachiwa baada ya kushikiliwa kwa siku sita, Julius Ssekitoleko, ameeleza nafuu anayoisikia baada ya kutoshtakiwa kwa sasa kwa kuwa amepatiwa dhamana huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Alikuwa nchini Japan kushiriki katika michezo ya Olimpiki, lakini baadaye aliambiwa kuwa hajafuzu kushiriki michuano hiyo na anapaswa kurejea nyumbani.

Badala yake aliacha ujumbe katika chumba chake akisema alitaka kuishi na kufanya kazi nchini Japan, kisha alitoweka.

Mwanasheria wale Phillip Munabi amesema polisi wanatazama ni kwa namna gani alisafiri kuelekea kwenye michezo ya Olimpiki 2020 bila kufuzu kushiriki michezo hiyo.

Kukamatwa kwake baada ya kuwasili nyumbani na kushikiliwa kulizua ghadhabu.



Waganda kwenye mitandao ya kijamii waliokuwa wakimuunga mkono mwanamichezo huyo wamesema kuwa kukosekana kwa ajira na fursa finyu nyumbani huweza kuwasukuma wanamichezo kutokomea kwenye nchi zilizoendelea.

Yeye si Mganda wa kwanza kutoweka katika matukio ya kimichezo ya kimataifa.

Mwezi uliopita, mchezaji wa rugby James Odong alitoweka jijini Monaco, wakati timu ya taifa iliposafiri kwenye michezo ya kufuzu Olimpiki.

Mwaka 2018 katika michezo ya Jumuiya ya Madola nchini Australia, wanamichezo kadhaa wa Kiafrika na maafisa kutoka nchi za Afrika, wakiwemo raia sita wa Uganda walitoweka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad