Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wa chuo Cha mafunzo ya Kijeshi Wilaya ya Monduli(TMA) Mkoani Arusha kwa tuhuma za mauaji ya Lais Lemomo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , amesema limetokea baada ya mwanajeshi huyu kumpiga risasi Lemomo akiwa anachunga Mifugo.
Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi pindi utakapokamilika taarifa kamili zitatolewa.
“Tukio hili lilitokea mnamo tarehe 12 mwezi huu majira ya jioni timu ya makachero ipo katika eneo la tukio na uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi itatolewa “amesema.
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Frank Mwaisumbe na Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli,Isack Joseph walifika eneo la mauwaji hayo ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya wafugaji na Jeshi.
Mwaisumbe alitoa pole Kwa familia na kuahidi uchunguzi wa tukio hilo itafanyika na Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
Katika hatua nyingine ACP Justine Maseli amesema jeshi la polisi linaendelea kumhoji mganga Mmoja wa kienyeji mkazi wa kata ya Sombetini kwa tuhuma za kumshawishi baba wa mtoto kumfanyia ukatilii dhidi ya mtoto wake.
“Mnamo tarehe nane mwezi wa saba mwaka huu tulitoa taarifa kuwa mtoto mwenye umri wa miaka minne alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na mwishoni kutelekezwa”ameongeza.
Kamanda Masejo amesema baada ya kumkamata na kumhoji mganga huyo alikubali kuwa kweli alimshawishi baba huyo kufanya hivyo na kumwambia endapo angefanya hivyo angepata utajiri katika shughuli zake anazozifanya