Waziri wa Maji Jumaa Aweso amekataa ombi la Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange lakutaka kupumzika kutoka katika nafasi hiyo mara baada ya utendaji wake mzuri katika mamlaka hiyo.
Waziri Awesoo amekataa ombi kupitia mkutano wa DAWASA wa kufunga mwaka 2010/21 na kuanza mwaka 2021/22 ambapo amesifu kazi kubwa iliytofanywa na DAWASA chini ya Mwenyekiti huyo huku akibainisha kuwa Wizara inahitaji wakurugenzi wa mamlaka za maji wa aina hiyo.
“Mhe. Mwenyekiti wa bodi ulinipigia simu juzi ukaniomba umefanya kazi kubwa sana na katika kipindi hichi uliomba kwa ridhaa yako ulituomba upumzike kwa kazi hii nzuri hakuna kupumzika tunaomba uendelee,” amesema Mhe. Aweso.
Pia Mhe. Aweso ameeleza kutokuridhishwa na gharama zisizoeleweka katika uunganishiwaji wa maji huku akiitaka DAWASA kushughulikia suala hilo ili wizara iweze kuwasilisha gharama stahiki kuunganishiwa maji kwa wananchi.
“Bado siridhishwi na gharama za uunganishwaji maji kwa wananchi, nataka mje na standard, mwananchi ilikuunganishiwa maji kiasi gani, naomba mje na gharama halisi na hili jambo naomba DAWASA mkalifanyie kazi na katika eneohili kusiwe na ubabaishaji,” amesema Mhe. Aweso.
Aidha, Aweso amewausia watumishi na watendaji katika mamlaka na taasisi zote za maji kuwa na kauli nzuri kwa wataje wao kwani wao ndio mabosi zao hivyo wanapaswa kuthaminiwa kutokana na mchango wao mkubwa katika maendeleo ya mamalaka hizo