STAA mkubwa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu anasema kuwa, watu wajifunze mazuri kutoka kwake, lakini wasiwe wanapenda kumuiga kila kitu kwa sababu wataumia.
Wema anasema kuwa, kila wanachopenda kumuiga kina madhara yake siku zote hivyo wajifunze au vitu vingine waviangalie tu na kuviacha vipite kama vilivyo.
Katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA, Wema anasema kuwa, anawaona watu wengi wakijaribu kumuiga hata pasipostahili.
Anasema kuwa, wapo wengine wanataka kuwa kama alivyo ndani ya siku moja, jambo ambalo haliwezekani kwani wakifanya hivyo wataumia.
“Jamani mtu anataka kuwa kama mimi kwa siku moja, hawajui mtu amepitia msoto gani mpaka kufikia hapo alipofikia, ni jambo la kushangaza sana hivyo kama wanataka kuwa kama mimi, wawe wavumilivu wa kila kitu maana wasifikiri kila kitu ni rahisi tu, haiwezekani na siyo kila kitu cha kuniiga maana mtu atajikuta anaumia bure,” anasema Wema ambaye baada ya kusemwa mno kwa sababu ya kukondeana, hivi sasa mwili umeanza kurudi.