Bananga "Namuunga Mkono Manara Hata Mimi Ningeambiwa Nichaguliwe Marafiki Ndio Nipewe Milion 4 Ningekataa"



Ameandika # bananga
👇👇👇👇
"Nimesikia kama wengi wetu mlivyosikia kuhusu mgogoro kwenye club yetu.
Nimechagua kusimama na @hajismanara pamoja na mapungufu yake.
Kwa nini;

1-Kazi yake ya usemaji ameifanya kwa weledi mkubwa. Leo ndio nembo ya wahamasishaji wakubwa wa soka.

2-Possibly ndiye binaadamu anayetukanwa sana kuhusu Simba inapofanya vibaya (ushahidi ni ktk mitandao ya kijamii) anatukaniwa mpk hali yake (albinism). Hivyo suala la Haji kuisaliti Simba NITAKUWA WA MWISHO KUAMINI.

3-La kupangiana marafiki kisa tofauti za kiitikadi, kidini, kihali, kishabiki HUO NI USHAMBA. Aachwe aishi maisha yake bora tu kazi aliyopewa anaifanya sawasawa.

Lakini kosa la Uongozi wa Simba hili la mgogoro wanalijua si leo wala jana, lina muda maana toka msimu uliopita Haji alitamani kupumzika, we smell the rat that time baadae mkubwa @moodewji akashow up likapoa, kumbe halikwisha. Tujifunze kumaliza migogoro badala ya kupooza maana itawaka tena.

Haji hata kama umekosewa ila UMEKURUPUKA SANA KUROPOKA, Sheikh mtoto wa kike yule, mrembo yule, umetumia silaha kubwa sana, maneno makali kwenye jambo lililotaka hekima. @bvrbvra amechukua pointi 3 muhimu kwa kuamua kukaa kimya. Maneno ya kumwambia Mwajuma Ndala Ndefu unamwambia Babra? Ukiambiwa ulikuwa unataka mengine ukagomewa unatokaje humo kaka? Kulikuwa na njia bora ya ww kuwasilisha kinachokuuma na WENGI WANGESIMAMA NAWE kuliko njia hiyo hii uliyoichagua.

Nimesikia clip ya kilio chako Haji, nimejikuta machozi yamenitoka. Inauma sana mahali ulipotoa kila ulichoweza kutoa UNAPUUZWA NA KUDHARAULIWA eti kwa kuwa kuna mmoja kama si wachache wanaamini huna maana. Unapitia ninachopitia licha ya kuwa ni field tofauti (Soka na Siasa). Ila ww kulipwa tsh 700,000 kwa mwezi HUKU NI KUKUDHALILISHA. Umefanya makubwa mnooooo kulingana upewacho. Simba hiyo hapana. Lakini kama alivyosema Hanspope kwa ulipewa mkataba wa tsh milioni 4 ila kwa masharti ya kuachana na watu fulani HATA MM NINGEKATAA. Maisha ni haki yako, ishi upendavyo na uwapendao bora HUVUNJI SHERIA.

Kuna maisha baada ya Simba, kuna wakati mwingine utakuja Simba. Kila aliyeko Simba ANAKIRI UMAHIRI WAKO.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad