Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima amesema watanzania wanatakiwa kuwa na imani na chanjo ya uviko 19 iliyoletwa nchini kwani ni salama na imethibitishqa na Shirika la Afya duniani(WHO).
Ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya uzinduzi wa chanjo ya Kinga ya Uviko 19 utakaofanyika kesho kwa Rais wa Jamhuri ha Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kuchanjwa.
Gwajima amesema, kesho Rais Samia atazindua chanjo hiyo kwakuwa mtanzania wa kwanza kuchanjwa baada ya Tanzania kupokea chanjo hizo kutoka nchini Marekani.
“Rais wetu ameonesha ushujaa na Utayari wake wa kuongoza utoaji wa chanjo ya Uviko 19 na hili tunalisema kama uthubutu na uzalendo kwa taifa lake,”amesema Gwajima.
Amesema, watanzania wanatakiwa kuwa na imani na chanjo hiyo kwani ni salama na inamtasaidia mwananchi kupambana na wimbi la tatu la ugonjwa huo ambao umeshika kasi duniani.
Amesema, Watakaoanza kupata chanjo ni makundi maalumu wazee kuanzia miaka 50, wagonjwa ndio wanaoshambuliwa na magonjwa kama kisukari, moyo na mengine
Gwajima amesema, serikali wamedhamiria Kuimarisha huduma ya elimu ya chanjo ya uviko 19 lengo likiwa ni kila mwananchi popote alipo apate elimu, kusikia na kupata ufafanuzi wa kisayansi.
Amesema, Watakaoanza kupata chanjo ni makundi maalumu wazee kuanzia miaka 50, wagonjwa ndio wanaoahambuliwa
“Baada ya uzinduzi wa kesho wa Rais Samia utafuata wa kila mkoa itakayokuwa inaongozwa na wakuu wa mikoa na chanjo hizo zitatolewa kwa makundi maalumu,”amesema.
Naye moja ya wataalamu wa Kinga kutoka Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Prof Karim Premji Manji amewaondoa hofu watanzania kuwa chanjo iko salama, ingawa watu wamekuwa wanahoji muda wa kutengenezwa kwa chanjo hiyo.
“Chanjo inaweza kutengenezwa ndani ya muda mfupi, mambo yamebadilika na sayansi imezidi kubadilika hususani kwa magonjwa yanayoua haraka kama ebola, uviko na mengineyo,”amesema Prof Manji
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Leonard Subi amesema Chanjo inaweza kutengenezwa ndani ya mwaka mmoja na inatengenezwa kuzingatia mfumo sahihi wa kisayansi.
Amewataka wananchi kuchanjwa kinga hiyo ili kumsaidia pia atakapopata maambukizi hayatakuwa makali na kumfanya kushindwa kwenda katika shughuli zake za kila siku.
Kufikia tarehe 22 Julai, 2021 jumla watu 4,127,963 walishapoteza maisha duniani huku 191,773,590 wakiwa wamethibitika kuwa na maambukizi ya UVIKO 19, upande wa Afrika kwa tarehe hiyo hesabu ya walioambukizwa lishafikia 4,583,414 na vifo 108,056.