China yakataa WHO kuchunguza mara ya 2 chanzo cha COVID-19



China imesema haitawaruhusu maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO wa kufanya awamu ya pili ya uchunguzi kuhusu chanzo cha maradhi ya COVID-19 kwenye maabara za nchini humo. 
Naibu mkuu wa tume ya kitaifa ya afya nchini China Zeng Yixin amesema hayo hii leo na kuongeza kuwa ni mpango wa WHO umejaa lugha ambayo haiheshimu misingi ya sayansi huku akipuuzilia mbali nadharia kwamba virusi hivyo vilitokea kwenye maabara za Wuhan mji ambako viligunduliwa kwa mara ya kwanza. 

Wameongeza kusema kuwa maabara hizo hazina virusi vinavyoweza kumuathiri mwanadamu moja kwa moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad