China yashutumiwa kwa udukuzi wa Kimataifa



Nchi ya Marekani na washirika wake, wameishutumu China kwa kuendesha kampeni ya kimataifa ya upelelezi wa mitandaoni.



Marekani iliungana na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Umoja wa Ulaya, Australia, Uingereza, Japan, Canada na New Zealand katika kulaani udukuzi huo, ambao Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema unaweka kitisho kikubwa kwa usalama wa kiuchumi na kitaifa.

Sambamba na hilo, Wizara ya Sheria ya Marekani imewashitaki raia wanne wa China, maafisa watatu wa usalama na mtaalamu mmoja wa udukuzi, kwa kuzilenga kampuni, vyuo vikuu na mashirika ya serikali nchini Marekani na kwingineko ulimwenguni. Msemaji wa ubalozi wa China mjini Washington Liu Pengyu, aliziita tuhuma hizo dhidi ya China kuwa za kijinga.

By-BAKARI WAZIRI


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad