Nessebar ni mji wa zamani uliopo kandakando ya kisiwa. Kisiwa hicho kipo nusu maili ya nyumba moja ya mvuvi iliopo juu ya mlima karibu na pwani ya taifa la Bulgaria ambayo imeunganishwa na daraja katika eneo hilo.
Mji huo uliopo katika magofu ya nyumba yenye zaidi ya miaka 3000 unatambuliwa na shirika la Unesco kama turathi za kitaifa.
Unapotembea katika mji huo wa zamani , nyumba za wavuvi wa karne ya kumi na tisa zipo karibu na kanisa la mtakatifu Medieval Stephen , ambalo limerembeshwa na picha za Yesu zinazovutia na vipande 1000 za picha kutoka kitabu cha Agano jipya.
Pia kuna magofu yaliyochimbuliwa ya Kanisa la Stara Mitropolia, kanisa kuu ambalo lilianzia karne ya 5 wakati lilipokuwa moja ya miji muhimu zaidi ya biashara ya enzi za Byzantine kwenye pwani ya Bahari Nyeusi.
Wanaakiolojia na wavuvi wa eneo hilo wamegundua sanduku moja la zama za kale. Magofu ya nyumba za kale na ufinyanzi wa Uigiriki ulianza kabla ya kuwasili kwa Warumi. Pia, kuna ukuta uliojengwa na waanzilishi wa jiji hilo, Thracians, watumizi wa farasi ambao walitawala rasi ya Balkan zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.
Lakini ili kuweza kupata vitu vya kale vinavyoshangaza zaidi , utahitajika kuondoka katika kisiwa hicho na kuelekea kandokando ya bahari hiyo. Hivi majuzi , utafiti uliofanywa baharini katika maji ya bahari nyeusi uligundua vipande vya vitu vya kale ambavyo havijawahi kuonekana katika historia.
Ujumbe wa manowari uliotumwa kufanya utafiti huo uligundua meli ya wafanyabiashara pamoja na meli kadhaa za kivita chini ya bahari hiyo, ikiwemo meli ya wafanyabiashara wa Ugiriki iliozama takriban miaka 400 kabla ya ujio wa Kristo.{ BC}.
Na miongoni mwa mabaki hayo ya meli , ni ushahidi mpya unaodai kwamba miaka 7000 iliopita, baadhi ya wataalamu waliamini kwamba bahari nyeusi ilikuwa ziwa dogo. Sampuli za kijiolojia zilizochimbwa katika sakafu ya bahari hiyo hatimaye zimetatua siri kuhusu mafuriko yalitokea na kuwacha hadithi ya nabii Noah na Safina yake.
Zdravka Georgieva, Mwanaakiolojia wa baharini ambaye amekuwa akifanya utafiti chini ya bahari katika eneo la Sozopol , Bulgaria alizaliwa katika kisiwa cha Nessebar na akasoma akiwa muogeleaji wa maji yaliopo ufuoni mwa bahari nyeusi.
”Nilitaka kujua kile kilichokuwa chini, nini kilikuwa chini ya maji hayo” , alisema Georgieva, ambaye kwa mara ya kwanza alisikia kuna mabaki ya meli ambazo hazijagunduliwa katika Makavazi ya Nessebar ambayo yanamiliki vitu kadhaa vya zamani.
Nilijua kwamba kutoka katika makavazi haya, na kutoka kwa wakazi wa eneo hili kulikuwa na vitu vya kale katika eneo hilo ambavyo nilitaka kuvigusa na kuvichunguza kwa ukaribu.
Baada ya kusomea katika chuo kikuu cha Southampton kuhusu uakiolojia wa baharini nchini Uingereza, Georgia alifanikiwa kutimiza ndoto yake kwani aliajiriwa katika kazi aliotaka kufanya akiwa miongoni mwa Wanaakiolojia wa mradi wa baharini ambao ulilenga kubaini jinsi bahari na maeneo yanayoizunguka yamebadilika tangu zama za barafu kwa kuchunguza sakafu ya bahari hiyo.
Kundi hilo lililoshirikisha wataalamu wa Ubelgiji na wenzao wa Uingereza lililoongozwa na Profesa Jon Adams wa chuo kikuu cha Southampton kwa ushirikiano na kituo cha uchunguzi wa chini ya maji ya bahari, liligundua meli ya miaka 2400 ya wafanyabiashara wa Ugiriki pamoja na mabaki mengine ya meli 60 yaliopatikana katika kina kirefu cha bahari hiyo.
Wakati mashine ya ROV 3D iliposkani eneo hilo meli hiyo ya zamani ilipatikana imelala upande mmoja , mlingoti na usukani ulikuwa ukionekana wazi, pamoja na madawati na chombo kikubwa cha kauri katika eneo hilo.
Georgieva aliutaja ugunduzi huo wa kuvutia zaidi – kufikia sasa.”Georgieva anakubaliana na wanaakiolojia wenzake wa majini kwamba tunaelekea katika miaka ya ugunduzi katika bahari nyeusi. Wote Georgieva na Ballard wanasema kwamba uvumbuzi wa maji ya bahari yenye kina kirefu unatoa usahidi mpya kuhusu siri kuu.
Katika kitabu cha mafuriko ya Noah kilichoandikwa na William Ryan 2000 na Walter Pitman , wanajiolojia wa wa majini wanaamini wamegundua chanzo cha mafuriko hayo ambayo yaliharibu miji ya zamani iliokuwa ikipakana na bahari ya Mediterenia na bahari nyeusi miaka 7,600 iliopita.
Hadithi hiyo imekuwa maarufu kote duniani kama vile jinsi hadithi ya Safina ya Noah ilivyoandikwa katika kitabu cha Biblia na kile cha Quran. Kulingana na Ryan na Pitman, takriban miaka 20,000 iliopita , kile kinachotajwa kuwa bahari nyeusi ilikatwa na milima kutoka kwa bahari ya Mediterenia.
Nadharia ya Mafuriko ya Noah inadai kwamba kuyeyuka kwa barafu za polar kulisababisha maji ya Mediterania kuongezeka , ambayo yalitengeneza njia katikati ya milima kabla ya kusababisha mafuriko mabaya ya maji ya bahari, yenye nguvu mara 200 kuliko maporomoko ya maji Niagara.
Katika kinpindi cha miezi michache , inakadiriwa , bahari nyeusi ilifinika ardhi yenye ukubwa sawa na Ireland kwa siku . Ballard mwaka wa 2000 alitumai kuelezea nadharia ya Ryan na Pitman, wakati alipogundua mafuriko hayo na majumba waliokuwa nayo kandokando ya bahari nyeusi iliopo pwani ya Uturuki.
Anaamini kwamba ugunduzi huo utasaidia kusema ukweli kuhusu mafuruko hayo. Lakini ramani ya bahari nyeusi ina maelekezo tofauti , anaelezea Georgieva. Wanajiolojia na wataalam kutoka kituo cha utafiti wa baharini mjini Southampton , wanasema kwamba hakuna ushahidi kuunga mkono nadharia hiyo, alisema.
”Kile tulichokusanya hakithibitishi mafuriko hayo yasio ya kawaida. Data inasema kwamba kuna uwezekano maji ya bahari yaliongezeka”.
Hatahivyo, Ballards anaiita bahari nyeusi kama eneo zuri lenye historia ambalo lenye mafunzo mengi zaidi ya historia ya Safina ya nabii Noah.
Bahari nyeusi ina uhusiano wa na biblia kuhusu Jason na Argonauts. Bulgaria ina history kubwa ya kiakiolojia ya Warumi , Ugiriki na watu wengine wa kale.