Hivi Ndivyo Wekundu wa Msimbazi Simba SC Walivyokata Ngebe za Yanga


Wekundu wa Msimbazi Simba SC wametwaa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Watani wao wa Jadi, Yanga SC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika, Kigoma

Bao pekee la Simba SC limefungwa na Kiungo Mkabaji wa Kimataifa wa Uganda, Thadeo Lwanga baada ya kona safi iliyopigwa na Nyota, Luis Jose Miquissone katika dakika ya 80 ya mchezo huo.

Simba SC rasmi imekata ngebe zilizoenea kila kona ya nchi kuelekea mchezo huo uliopigwa Magharibi mwa Tanzania, katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia dakika zote 90, Kiungo Mkabaji wa Yanga SC, Mukoko Tonombe alionyeshwa Kadi Nyekundu katika kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kiwiko, Mshambuliaji wa Simba SC, John Bocco.

Kupindi cha Pili, Simba SC waliukama mchezo huo kwa kucheza kwa kasi na kushambulia kwa zaidi kutokana na kadi nyekundu ya Mukoko iliyowaathiri Young Africans SC katika kipute hicho.

Rasmi Simba SC wametawazwa kuwa Mabingwa wa Michuano hiyo kwa mara ya tatu katika misimu tofauti kwa mara ya kwnza walitwaa mbele ya Mbao FC katika dimba la Jamhuri, Dodoma, mara ya pili Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga dhidi ya Namungo FC mara hii ni Lake Tanganyika, Kigoma dhidi ya Yanga SC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad