Kauli ya Simba kuhusu kumuuza Miquissone ''Sisi sio kama Yanga Mchezaji Akipata Sehemu Nzuri Tunamruhusu"

 


Uongozi wa Klabu ya Simba umesema hautomzuia mchezaji yeyote kuondoka msimbazi katika dirisha hili la usajili iwapo bodi itaridhia kwa maslahi ya pande zote mbili

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba upande wa Wanachama, Mwina Kaduguda katika moja ya Mkutano wa Wekundu wa Msimbazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi upande wa Wanachama, Mwina Kaduguda amesema kuwa klabu yao si kama watani zao Yanga ambao amejinasibu kuwa wamekuwa na tabia za kuwazuia wachezaji wao kusajiliwa na klabu zingine nje ya nchi.

Kaduguda amesema kuwa ni kweli wamezisikia taarifa za kuhitajiwa kwa mchezaji wao Luis Miquissone na klabu ya Al Ahly ya Misri ambayo inatajwa kuwania saini ya raia huyo wa msumbiji.

''Sisi sio kama Yanga, kama mchezaji amepata maslahi sehemu nyingine hatuwezi kumzuia,wapo wachezaji ambao wameomba kuondoka na tumepata maombi muda mrefu tutawauza kwakuwa hatuwezi kumzuia mtu kufanya maendeleo'

''Kuhusu Miquissone liko vizuri, tutalitolea ufafanuzi hapo baadaye, kama Klabu itaamua na iwapo ataenda Al Ahly kwanza ni kujenga mahusiano mazuri na Klabu kubwa Afrika, kama unavyojua CEO wetu alikwenda kufanya ziara kule na kujifunza namna ya uendeshaji wa klabu''Mhina Kaduguda akizungumza na East Africa Radio.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad