Kimanuka! Maandamano ya Kumtoa Zuma Jela Yapamba Moto, Magari Yachomwa




Maelfu ya waandamanaji wanaotaka kuachiwa kwa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, wameingia mitaani na kuchoma magari kadhaa katika Jimbo la Kwa Zulu Natal, ikiwa ni hatua ya kuishinikiza serikali kumuachia kiongozi huyo wa zamani.

 

Zinhle Mngomezulu, msemaji wa Kikosi cha Ukaguzi na Usalama Barabarani katika Jimbo la KwaZulu-Natal amesem magari kadhaa ya mizigo yamechomwa moto na waandamanaji kuanzia usiku wa Ijumaa na Jumamosi asubuhi, na kusababisha hali ya taharuki katika jimbo hilo.



Msemaji huyo amesema miongoni mwa magari yaliyochomwa moto, ni magari yanayosafirisha mafuta, hali iliyosababisha barabara kadhaa kutopitika jimboni humo.

 

Katika video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, magari mbalimbali yanaonekana yakiwa yanateketea kwa moto huku waandamaji wakikimbia huku na kule, wakiimba nyimbo na kubeba mabango yanayoshinikiza kuachiwa kwa Zuma.



Waandamanaji wengine waefunga barabara wa kuchoma magudumu, katika maeneombalimbali ya Jimbo la Kwa Zulu Natal, mahali alikozaliwa Zuma, wakishinikiza aachiwe kutoka gerezani.

 

Siku kadhaa zilizopita, Zuma mwenye umri wa miaka 79 alikutwa na hatia ya kuidharau mahakama baada ya kutohudhuria mahakami kusikiliza kesi ya ufisadi inayomkabili na kuhukumiwa kifungo cha miezi 15 jela.



Inaelezwa kwamba sababu kubwa ya Zuma kutohudhuria mahakamani, ilikuwa ni msimamo wake wa kutaka jaji anayesikiliza kesi hiyo abadilishwe kwa sababu hakuwa na imani naye, jambo ambalo mahakama ililikataa na kusababisha mvutano huo.

 

Jumatano usiku, Zuma alijisalimisha mwenyewe katika Gereza la Estcourt kwa ajili ya kuanza kutumikia kifungo chake hicho.



Jeshi la polisi nchini Afrika Kusini, limesema mpaka sasa limewakamata watu takribani 27 kwa kosa la kuandamana na kusababisha vurugu katika Jimbo la Kwa Zulu Natal. Msemaji wa Polisi, Jay Naicker amesema jeshi la polisi linaendelea kukabiliana na maandamano hayo lililoyaita haramu na yanayovunja sheria.

 

Wakati hayo yakiendelea, Taasisi ya Jacob Zuma Foundation imesema ina wasiwasi mkubwa kutokana na kufungwa kwa Zuma kwa sababu ya hali yake ya kiafya, hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mlipuko wa ugonjwa wa Corona, huku pia ukiwa ni msumu wa baridi kali nchini humo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad