Kimenuka..Meninah Matatani Kifo Cha Mumewe



MSANII wa filamu na Bongo Fleva, Menina Attick ‘Meninah’, ameingia kwenye mkasa na utata mzito baada ya kifo cha mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Yona au Musa.


Kwa mujibu wa ndugu wa Musa, kijana wao alifariki dunia siku chache zilizopita, lakini tuhuma nzito zikishushwa kwa Meninah anayekimbiza na wimbo wake mpya wa Nyumba Kubwa.


Ndugu hao waliliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, Meninah alikuwa hamjali mumewe huyo wa ndoa ilihali akiwa mgonjwa hadi mauti yalipomkuta.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mtu wa karibu wa marehemu alisema kuwa, kitendo alichofanya shemeji yao kilikuwa ni cha kuumiza mno kwani alikuwa akimfungia ndani ndugu yao bila hata kumfanyia usafi kwa kuwa alikuwa mgonjwa.


“Yaani inatuumiza sana maana hata kuumwa kwa ndugu yetu tumejua dakika za mwishomwisho kabisa kwa sababu Meninah alikuwa anamficha wala hatuambii chochote na huku ndugu yetu hapati huduma inayostahili wakati alikuwa mgonjwa,” alisema ndugu huyo.


Aliendelea kufunguka kuwa, kwanza Meninah alimpa mashariti ndugu yao huyo, asiweke wazi kama amemuoa wala hata kuposti picha mitandaoni kama ni mkewe maana hakutaka watu wake wengine wanaomsaidia wajue kama ameolewa.


“Yaani hata ndoa ilifungwa kwa siri maana watu wote waliokuja kwenye harusi, simu zao zote ziliwekwa kwenye sinia moja ili picha zisipigwe hivyo hata cheti cha ndoa hakikuonekana; yaani hatukujua kwa nini alifanya hivyo,” alisema.


Alisema kuwa, ndugu yao alikuwa yupo chini kwa Meninah pamoja na kwamba alimsaidia mno wakati anahangaika na kumaliza ile ishu ya koneksheni yake na Mwijaku.


“Ndugu yetu alimsaidia sana Meninah mpaka yale mambo yake na Mwijaku yakapoa, lakini hakumthamini kabisa; yaani sisi tunamfuata kumpeleka Hospitali ya Temeke, tukamkuta hajiwezi kabisa, alishachoka na kingine ni stresi zilimfanya apoteze uhai mapema,” alidai ndugu huyo.


Gazeti la IJUMAA lilizungumza na baba wa marehemu Musa ambaye alisema asingependa kulizungumzia suala hilo kwani ameamua kumuachia Mungu.


Gazeti hili lilimtafuta Meninah kwa njia ya simu, lakini simu yake haikuwa hewani tangu kutokea kwa ishu hiyo hivyo jitihada zinaendelea.


Meninah ambaye pia ni MC maarufu Bongo anayekiwasha kwenye Tamthiliya ya Jua Kali na Yona au Musa walidaiwa kufunga ndoa mwaka 2017 na kujaaliwa mtoto mmmoja.Mwili wa Yona ulipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kijijini kwao, Mkata, Handeni jijini Tanga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad