Shirika la Afya Duniani WHO limesema kirusi kipya cha corona kiitwacho delta kipo kwenye Nchi 10 kati ya 16 za Afrika ambazo covid 19 imesambaa kwa wingi.
WHO imesema bara la Afrika limeathirika vibaya zaidi na janga la virusi vya corona wiki hii ila hali bado itakuwa mbaya zaidi huku wimbi la tatu la maambukizi likishika kasi.
Dokta Matshidiso Moeti ambaye ni mkurugenzi wa WHO Afrika amesema maambukizi katika bara la Afrika yanaongezeka sana kila baada ya siku 18 ikilinganishwa na wakati uliopita.
Moeti amesema ongezeko hili la maambukizi halitoisha hadi baada ya wiki kadhaa ambapo katika wiki iliyoisha July 4 pekee, Afrika ilirekodi zaidi ya maambukizi laki mbili na elfu hamsini ikiwa ni ongezeko la asilimia 20.