Kisinda, Yacouba Waongezewa Makali Yanga





KATIKA kuelekea Kariakoo Dabi, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amewaongezea program ya mazoezi wachezaji wake akiwemo Tuisila Kisinda na Yacouba Songne ili kuhakikisha anapata ushindi.

 

Kariakoo Dabi hiyo inahusisha Simba dhidi ya Yanga, mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi, kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni.Timu hizo katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa uwanjani hapo, zilitoka sare ya bao 1-1.



Mmoja wa mabosi wakubwa wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, Nabi tangu juzi timu hiyo ilipoingia kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni, Dar, alianza program zake za mazoezi kwa kufanya mara mbili, asubuhi na jioni ili kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo mgumu.

 

Alisema kuwa kocha huyo asubuhi anawafanyisha mazoezi ya fitinesi na jioni ya kimbinu jinsi ya kufunga mabao na kulinda lango lao.

 

“Tangu timu ilipoingia kambini, mazoezi yanafanyika mara mbili kwa siku kwa maana ya asubuhi na jioni ili kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.

 

“Program hiyo ya mazoezi inawahusisha wachezaji wote waliokuwepo kambini, ikihusisha jinsi ya kulinda goli na kushambulia ndani ya wakati mmoja.“

 

Wachezaji waliokosekana katika mazoezi hayo ni Niyonzima (Haruna) ambaye ana malaria na Sarpong (Michael), Metacha (Mnata) na Moro (Lamine) ambao wamesimamishwa kwa utovu wa nidhamu,” alisema bosi huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad