KOCHA mkuu wa kikosi cha Yanga, Nasriddine Nabi ameshindwa kutokea kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa fainali wa kombe la Shirikisho, dhidi ya watani wao Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma…(endelea).
Mchezo huo, utafanyika kesho Jumapili tarehe 25 Julai 2021, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, kuanzia saa 9:30 alasiri.
Katika ratiba ya siku ya leo Jumamosi, iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ilionyesha kocha wa Yanga alitakiwa kufanya mkutano na wanahabari kwenye moja ya kumbi za Uwanja wa Lake Tanganyika majira ya saa 5 asubuhi, mara baada ya Simba kumaliza saa 4:30.
Wachezaji wa Yanga wakiwasili Kigoma
Kocha huyo alishindwa kutokea pamoja na nahodha wa timu hiyo na badala yake alimtuma kocha wa makipa Razak Siwa katika mkutano huo, ambaye aliondolewa na Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo.
Aidha, katika makubaliano yaliyofanyika hapo awali kati ya klabu hizo mbili na TFF, ni kuleta makocha wakuu kwenye mkutano huo pamoja na manahodha na sio mtu mwengine.
Katika hatua nyingine, kikosi cha Yanga, majira ya saa 10 kitatembelea Uwanja huo (Pitch visiting), na baada ya hapo kitaelekea kufanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Chuo cha Hali ya Hewa