Stori ya chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 imekuwa gumzo duniani kote, na sasa inatishia kuhatarisha ajira za wale waliogoma kuchanjwa.
Makampuni makubwa ya huduma za tehama duniani, Google, Facebook na Netflix, wameweka wazi kuwa hawatokuwa na nafasi ya kuendelea kufanya kazi na watu ambao hawajapata chanjo ya ugonjwa wa Covid-19.
Inaripotiwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Google Sundar Pichai amewatumia barua pepe (email) wafanyakazi wake wote akiwapa taarifa kuwa watarudi rasmi kufanya kazi ofisini ifikapo October 18, na kuwa ikifika tarehe hiyo kila mfanyakazi anatakiwa awe amepata chanjo na awe na uthibitisho.
#Facebook nao wamechukua hatua hiyo hiyo wakitoa tamko kuwa kwa mtu yoyote anayetamani kufanya kazi na kampuni hiyo anatakiwa aambatanishe pia na cheti chake cha uthibitisho wa chanjo ya Covid-19 kwenye maombi yake ya kazi.
Nao #Netflix wameweka wazi agizo lao kwa wafanyakazi wake wanaotaka kuendelea na shughuli za uzalishaji filamu kwenda kwanza kuchanjwa ndipo shughuli zingine ziendelee.
Mataifa mengi ya Ulaya na Asia yameweka misimamo yake mikali juu ya wale waliogoma kuchanjwa chanjo ya Covid-19 ikiwemo kuwakataza kununua chakula kwenye Supermarket mbalimbali mpaka watakapopata huduma hiyo.