Kwa Mabosi Hawa Yanga, Kuna Mtu Anapigwa




SURA mpya za viongozi wa Baraza la Wadhamini wa Klabu ya Yanga ni ishara tosha wamedhamiria kufanya vema katika msimu ujao ikiwemo kutwaa makombe.

 

Baraza hilo jipya linaundwa sura mpya tatu kati ya hao watano kati ya hao wanajua vizuri fitna za soka ndani na nje ya uwanja, hiyo huenda ikawa na faida kubwa kwao katika msimu ujao.

 

Tofauti na kuzijua fitna, pia wadhamini hao wana nafasi kubwa za uongozi serikalini katika uongozi. Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla ndiye aliwatangaza wadhamini hao katika mkutano wake mkuu walioufanya wiki mbili zilizopita kwenye Ukumbi wa DYCCC, Changombe jijini Dar es Salaam.

 

Wadhamini wanaoongozwa na Dk Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango aliyepewa nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu.



Nchemba ndiye aliyefanikisha usajili wa kiungo mkabaji Salum Abdallah ‘Fei Toto’ akiwa anaichezea Singida United ambayo alikuwa anaimiliki waziri huyo iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Bara.

 


Waziri huyo alipambana kuzima jaribio la watani wa Simba waliokuwa kwenye vita kubwa ya kumsajili kiungo huyo.

 

Mwingine ni Abbas Tarimba ambaye Mbunge wa Kinondoni, Dar pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, hivyo analifahamu vizuri soka la hapa nchini.

 

Geoffrey Mwambe yeye ni Waziri wa Uwekezaji, kwa kupitia nafasi yake aliyokuwa nayo atasaidia timu hiyo katika mambo mbalimbali ili kufanikisha malengo yao ya kuchukua makombe.

 

Pia yupo Waziri wa Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Kepteni George Mkuchika ambaye amekuwa katika kamati mbalimbali za Yanga kwa kipindi kirefu huku akiipambania katika mambo mbalimbali.Na Mama Fatma Karume ambaye mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, yeye amekuwa akiipambania Yanga kwa muda mrefu katika kufikia mafanikio yao na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa.

 

Mara kadhaa amekuwa akiisaidia na timu hiyo kila inapokwenda Unguja, Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi ambalo mwaka huu Yanga wamelichukua kwa kuwafunga Simba.Yupo aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega ambaye yeye hayupo kwenye Baraza hilo, alikuwepo kwenye kamati iliyopitisha katiba mpya ya Mfumo wa Mabadiiko wa klabu hiyo.

STORI: WILBERT MOLANDI,Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad