Madhara ya Upigaji Punyeto, na Namna ya Kuepuka





Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto.

Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k.

Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba “kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu” Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu.

Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 30 wameathirika na tatzo hili (chronic masturbation) na inakuwa ngumu kujinasua kutoka kwenye hili janga, kama wewe ni mmoja wapo na ulkuwa ukitafuta kwa mda mrefu ufanye nini ili uachane na tabia ya kupiga punyeto basi fatilia kwa makini makala hii.

MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO KWA MWANAUME
Haya ndio baadhi ya madhara ya kimwili ambayo yanaletekezwa na upigaji punyeto

1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME:
Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inalegea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umelegea.

2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO:
Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya tendo la ndoa na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mwenzake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kufanya tendo hilo.
Athari nyingine ni kama zifuatazo :

3.Uchovu wakati wote / Fatigue. Feeling tired all the time.
4.Maumivu ya nyonga / Lower back pain.
5.Kusinyaa kwa Nywele / Nywele kunyonyoka / Thinning hair / Hair Loss
6.Maumivu ya kende
7.Maumivu ya kiuno

Hayo ni baadhi ya nukuu zangu!
Kuna faida nyingi sana ambazo utazipata endapo utaachana na tabia ya upigaji punyeto na hiyo napenda iwe sababu ya wewe msomaji kuachana hicho kitendo.

Kuacha punyeto ama mtindo flani wa maisha inahitaji utambuzi, uamue na pia uweze kjicontrol wewe mwenyewe, inahitaji nguvu ya ndani yako kushinda vishawishi , zifuatazo ni njia ambazo utaanza kutekeleza ukiwa nyumbani kwako bila gharama yoyote na zitaanza kukupa matunda, lazima uwe mwaminifu kufuata kile ninachoelekeza maaana ni njia ambayo imewasaidia vijana wengi.

1.PATA MDA MWINGI WA KUPUMZIKA
Baada ya shuguli za kawaida haikisha unapata mda wa kupumzika, lala mapema ili uweze kuipa akili mda wa kuchambua na kutunza taarifa za muhimu na kufuta zile ziszo za muhimu. Hakikisha unalala mapema hapo ndipo utaongeza uwezo wa akili kuweza kupambana na hisia na mawazo mabaya.

2. MATUMIZI YA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KWA WINGI
Utafiti wa kisayansi unaonesha kwamba matumizi mazuri ya vyakula vya mbogamboga na matunda Husaidia kuongeza uwezo binafsi wa kujisimamia juu ya tamaa na mihemko mbalimbali, matumizi ya vyakula vilivyosindikwa (junk foods) ni chanzo cha kushindwa kujizuia na hapo safari yako ya kuachana na upigaji punyeto itakwama.

3. FANYA MAZOEZI NA USHUGULISHE MWILI
Maozezi yanasaidia mwili kutofikiria kufanya mambo machafu sababu mara nyingi unakuwa bize, akili inapokuwa inashugulishwa basi uwezekano wa kuleta fikra mbaya ni mdogo sana

4. ACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
Tafiti zinasema kwamba vijana wengi wenye umri kuanzia miaka 15 mpaka 30 ndo kundi kubwa lililoathirika kwa kutazama picha za pono, piacha au video za ngono huleta msukumo kwenye akili ili kuweza kujiridhisha na hivo hupelekea watu kupiga punyeto ili kukata ile kiu ya tamaa zao za mwili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad