Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amepiga marufuku hospitali na vituo vyote vitakavyotoa chanjo ya Corona kutoza pesa kwa wananchi.
Prof. Makubi amesema hayo leo Julai 30, 2021 wakati wa kuzindua zoezi la usambazaji chanjo ya Corona ya Janssen katika mikoa mbalimbali nchini katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali inatarajia kutoa chanjo hiyo kuanzia tarehe 3 Agosti 2021 siku ya Jumanne katika vituo 550 vya kutolea huduma katika mikoa yote Tanzania Bara. kwa kufuata makundi yenye vipaumbele wakiwemo, Watumishi sekta ya afya, watu wazima umri kuanzia miaka 50 na kuendelea pamoja na watu wenye magonjwa sugu.
By-BAKARI WAZIRI