Mlipuko umetokea kwenye bomba la mafuta chini ya maji katika Ghuba ya Mexico.
Mlipuko wa mita 78 chini ya bahari ulisababisha moto katika bomba la kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali Pemex.
Meli tatu za kuzima moto zilijaribu kuudhibiti mlipuko huo.
Moto juu ya uso wa bahari ulidhibitiwa baada ya masaa 5 ya kazi.
Mamlaka yamesema wanachunguza chanzo cha mlipuko uliosababisha moto.
Picha iliyopigwa wakati wa moto imeitwa "jicho la moto" kwenye mitandao ya kijamii