Mtaka: Msiwasikilize Sababu ya Uwaziri, Wanakula Viyoyozi

 
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthon Mtaka amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kumsikiliza yeye katika suala la elimu kwa kuwa yeye ndio anaishi nao kwenye kata zao.

 

Akizungumza na wananchi wa kata ya makulu leo Julai 12, 2021 amesema Mkoa wa Dodoma unakuwa wa mwisho kielimu kwa kuwa wazazi na walezi wamekuwa hawatoi kipaumbele katika elimu.

 

“kwa kuwa elimu ni kipaumbele changu kwenye jambo ili simtomsikiliza mtu wala mwanasiasa kwa kuwa wao wanawapangia watoto wenu wasome muda gani wakati wakwao wanasema shule za kimataifa…..”

 

Akitolea ufafanuzi kuhusu kauli yake, Mtaka amesema; Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile.

 

Naomba Radhi kwa wote waliokwazika, wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno “Waziri” lilipobeba hisia tofauti nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu.

 

Wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega,na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji, niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega….

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad