Mtihani Samaki wa Magufuli "Meli Kuuzwa Kama Chupa Chakavu"



WAKATI upande wa utetezi ukisubiri kutekelezwa kwa hukumu ya serikali kulipa fidia ya mabilioni ya shilingi kutokana na kukamata meli ya Tawariq 1 iliyokuwa na samaki mwaka 2009, maarufu Samaki wa Magufuli, serikali imesema inafikiria kuiuza meli hiyo kama chuma chakavu.

Meli ya Tawaliq 1 iliyokamatwa mwezi Machi, 2009 ikiwa na tani za samaki aina ya Jodari, iliyowavua katika Bahari ya Hindi ndani ya Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), wakati ilipoanza kuzama mahala ilipoegeshwa upande wa Kigamboni, mkoani Dar es Salaam. Picha nyingine; meli hiyo ikionekana kidogo jana, baada ya sehemu kubwa kuzama kabisa. PICHA: MIR6AJI MSALA/MAKTABA
Meli hiyo iliyodaiwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na samaki wenye thamani ya Sh. bilioni 2.074, ilikamatwa Machi 8, 2009 na boti ya askari wa doria wa Tanzania, Afrika Kusini na Botswana. Ilidaiwa leseni waliyokuwa nayo ilikuwa imemaliza muda wake Desemba Mosi, 2008.

Wiki iliyopita, Nipashe ilimtafuta Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, kuzungumzia suala hilo na alisisitiza utekelezaji wa hukumu iliyotolewa na mahakama unafanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Akizungumza na Nipashe kuhusu suala hilo jana, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, alisema:

"Ile meli bado iko pale ilipowekwa na 'actually' imeziba nafasi. Sisi tulianza kufikiria tuiuze kama chuma chakavu kwa sababu imeziba nafasi ambayo meli zingine zinaweza kuwekwa pale.


"Kwa ufafanuzi zaidi wa suala lenyewe, ninaomba nipate muda zaidi nione hatima ya serikali kupata fedha kwa maana tupige bei kama chuma chakavu ile meli iachie nafasi. Kwa hiyo, lile suala ni kama limeisha lakini bado halijaisha."

Machi 2017 kampuni ya uwakili iliyokuwa inawatetea 'Wachina wa Samaki wa Magufuli', ilitarajiwa kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Bahari kujua hatima ya madai yao ya meli ya Tawariq 1 yenye thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na zaidi ya Sh. bilioni mbili za samaki endapo hukumu haitatekelezeka.

Kampuni hiyo ilikusudia kuchukua uamuzi huo endapo hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti, mwaka 2014 haitatekelezeka.


Hatua huyo imefikiwa kutokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kwamba suala hilo lirudi Mahakama ya Kisutu ambako amri ya kurejeshewa vitu hivyo ilitolewa.

MAHAKAMA KUU

Uamuzi wa kuwataka wadai kudai utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya Kisutu ulitolewa na Jaji Munisi kutokana na hoja za Jamhuri.

Aliyekuwa Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis katika hoja za pingamizi alidai Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam haiwezi kusikiliza maombi ya ‘Wachina wa Samaki wa Magufuli‘ ya kutaka kurejeshewa meli yao iliyozama na samaki kwa sababu amri ya kurejeshewa ilitolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Upande huo wa Jamhuri ulidai mwombaji katika maombi hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tawariq, Said Mohammed, hana sifa ya kukabidhiwa mali hiyo, hivyo waliomba mahakama itupilie mbali maombi ya kutaka kurejeshwa meli ya Tawariq 1 na zaidi ya Sh. bilioni mbili za tani 296.3 za samaki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad