Mwisho wa Ubishi Ligu Kuu ni Leo, Mechi Tisa Kutikisa




LIGI Kuu Bara msimu wa 2020/21, inahitimishwa leo Jumapili kwa kuchezwa mechi tisa katika viwanja tofauti, huku vita kubwa ikiwa ni katika kuepuka kushuka daraja.

 

Timu nne ndizo zinapaswa kushuka daraja moja kwa moja ambazo zitakazomaliza nafasi ya 15, 16, 17 na 18, huku zile za 13 na 14, zikilazimika kucheza mechi za mtoano dhidi ya Pamba na Transit Camp za Ligi Daraja la Kwanza ili kutetea nafasi yao hiyo. Tayari Mwadui imeshuka daraja.

 

Katika mechi za leo, Coastal Union iliyo nafasi ya 14 na pointi 37, inakaribisha Kagera Sugar iliyo nafasi ya 11 na pointi 40.



Zote zinahitaji pointi tatu kujiweka salama.JKT Tanzania nao waliopo nafasi ya 15 na pointi 36, inapambana kupata pointi tatu kujiokoa na janga la kushuka daraja ambapo wanakwenda kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo nayo haipo salama ikiwa na pointi 39, ipo nafasi ya 13.

 

Ihefu wapo nafasi ya 16 wakikusanya pointi 35, wanaocheza nao KMC hawana presha kutokana na kushika nafasi ya tano wakiwa na pointi 45.



Ihefu inasaka pointi tatu leo, huku ikisikilizia matokeo ya JKT Tanzania na Coastal Union.Mbeya City wenyewe wanakwenda kucheza na Biashara United wenye uhakika wa kucheza kimataifa msimu ujao. Mbeya City wapo nafasi ya 12, pointi zao 39, wanataka kushinda ili kuwa salama zaidi.



Wengine waliokuwa kwenye majanga ni Gwambina wanaoshika nafasi ya 17 baada ya kukusanya pointi 34, wanacheza na Prisons iliyopo nafasi ya sita na pointi 43.Mechi zingine ni; Ruvu Shooting v Azam, Simba v Namungo, Dodoma Jiji vs Yanga na Polisi Tanzania vs Mwadui.

WAANDISHI: Hussein Msoleka, Hawa Aboubakhari na Johary Iddy

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad