SHABIKI wa Yanga ambaye amejizolea umaarufu mkubwa baada ya timu ya kuifunga Simba kwa bao 1-0, Julai 3, 2021, Mzee Mpili amesema mechi ya fainali ya Kombe la Azam Shirikisho kati ya Yanga na Simba, itakayochezwa katika Dimba la Tanganyika mjini Kigoma, Julai 25, 2021 tayari imeisha wanachosubiri ni siku tu wakabishiwe kombe lao.
“Mechi ya juzi nilijua tutashinda, hata kama Simba angetangulia kufunga ningesawazisha na kuongeza goli la pili.
“Mchezo wa Kigoma nimeshamaliza kazi, Kigoma hawatoki ng’ooo, niache kama nilivyo hawatoki. Wapeni habari kwamba Mzee Mpili amesema kama alivyowamenyeni Dar es Salaam na Kigoma mtawamenywa, tena magoli ya Kigoma ni ya kuhesabu.
“Tunajua Simba inajipanga kulipa kisasi kwenye mchezo wa Fainali ya FA lakini tayari wamechelewa Kigoma wanakufa tena na shughuli imeisha, tunawapiga tena.
“Nimepewa guarantee asilimia 100 kuwa Mechi ya Kigoma imeisha na tutashinda goli mbili kwenda mbele . Kama Wanasema jumamosi tulibahatisha sawa, Lakini Shughuli yote wataiona kigoma, hatuwezi kuliacha hilo Kombe,” amesema Mzee Mpili ambaye kwa sasa ana-trendi mitandaoni kila kukicha