Uhasama uliopo kwa sasa kati ya UAE na Saudia Arabia kuhusu uzalishaji wa mafuta ambao uneanza wiki hii ndio ulifanya mazungumzo kati ya wazalishaji wa mafuta kufutiliwa mbali.
Mzozo huo umeacha soko la mafuta katika hali ya kutatanisha kitu kilichopelekea bidhaa hiyo kupanda bei kwa mara ya sita mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa Wanachama 23 wanaozalisha mafuta na kuuza duniani walilazimika kuahirisha mkutano huo ghafla baada ya kujitokeza mzozo kati ya UAE na Saudia Arabia.
Tatizo lilianza wiki iliopita , wakati UAE ilipokataa pendekezo la wanachama wawili wa Opec+ Saudia na Urusi kuongeza usambazaji wa Mafuta kwa kipindi cha miezi minane ijayo.
UAE ilitaka kuanzisha mazungumzo mapya kuhusu nyongeza au punguzo la faida ya mafuta yake – ili kuweza kuipatia uhuru kuzalisha wa mafuta zaidi.
Hatahivyo, Saudia na Urusi walikuwa wanapinga wazo hilo.
Mazungumzo hayo yalichukua mwelekeo tofauti wakati mawaziri kati ya UAE na Saudia kuamua kutangaza tofauti zao hadharani.
Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na ushirikiano mkubwa kuhusu masuala ya kimkakati.