Watu wawili wamepoteza maisha mkoani Njombe baada ya kuingia na jiko la mkaa ndani ya chumba cha kulala kwa lengo la kupunguza baridi Mkoani Njombe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amethibitisha kutokea kwa tukioa hilo lililowakuta Benitho Mbatha (23) mpiga debe wa mjini Njombe na Jazila Said Mndendeule (27) mkazi wa Namtumbo.
“Baada ya kufariki hakuna mtua ambaye aligundua kama kuna watu wamefariki,tukio hili limetokea tarehe 17 mwezi wa saba majira ya saa tano na nusu huko mtaa nwa National Housing kata ya Njombe mjini wakiwa wamelala kwenye chumba kimoja”alisema Kamanda Hamis Issa
Aidha amesema “Sababu ya kifo chao inaonyesha wakati wakiwa hai waliweka moto wa mkaa kwa ajili ya kujihifadhi na baridi na huu mtindo wa kuweka mkaa kwa watu wa Njombe ndio mtindo wao”alisema Hamis Issa
Aidha kamanda Issa ametowa wito kwa wananchi wa Njombe kutumia njia nyingine kujikinga na baridi na si kuota moto kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya kwa kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maisha yao.
“Niwaombe wananchi wewe unaona Chumba chako ni kidogo na unatumia mkaa ndani hiyo ni hatari nyingine na huko lilikotokea tukio chumba ni kidogo na kina dirisha moja na dogo sana.Acheni kulala na jiko ndani ya nyumba sasa hivi ni hatari tafuteni nguo nzito nzito za kuzuia baridi lakini sio moto wa mkaa”alisema kamanda Issa
Kamanda Issa amesema tukio hilo ni la tatu kutokea mkoani Njombe kutokana na tukio jingine kumkuta dada mkazi wa Songea aliyekuwa mhudumu wa baa moja mjini Njombe kufariki ndani kwa jiko la mkaa huku mwingine akifariki wilayani Wanging’ombe kwa jiko la mkaa.
Amani Samsoni Mwalongo ni mmiliki wa Nyumba aliyokuwa akiishi marehemu Benitho Mbata huku akiwa ni mtu wa kwanza kushuhudia tukio hilo baada ya yeye kwenda kumtembelea marehemu na kuwaona wote wawili wakiwa wamefariki
“Lakini bado mimi nilifuatilia kwa majirani wanasema yule mwanamke alikuwa anaelekea Madaba,alikosa nauli na huyu kijana kwa kuwa yupo pale kwenye magari akamwambia njoo upumzike kwanza na kesho nitakusaidia nauli ya kukufikisha kwenu kwa hiyo hiki kitu kinahuzunisha sana”alisema Amani Samson
Kwa upande wao Majirani wanasema “Marehemu huwa anapenda sana kuja hapa na alikuja pia akachukua moto na akachukua shipsi Mayai akasema nina mgeni wangu huko ndani lakini siku baada ya siku tukashangaa haonekani mpaka tulipoona wanakuja polisi,lakini sio vizuri kwenda kulala sehemu usioijua kwa mfano hapo huyo mwanaume angefariki halafu angebaki mwanamke tayari angekuwa na kesi ya kujibu”alisema mmoja wa majirani.