PASTA mmoja wa Uganda alisherehekea kifo cha Nabii Temitope Balogun Joshua, almaarufu TB Joshua, akimtaja marehemu kama “mchawi mkuu barani Afrika.”
Kupitia video iliyosambazwa mitandaoni, Pasta Jackson Senyonga wa Kanisa la Christian Life, jijini Kampala, alisisitiza kuwa kifo cha TB Joshua ni ushindi kwa raia wa Nigeria na Waafrika.
Senyonga alimshutumu marehemu aliyeanzisha Kanisa la Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) dhidi ya “kuwatoa” wengi kafara.
“TB Joshua aliwatoa kafara watu wengi akidhani roho yake ina thamani kuu kushinda ya wengine,”
“Kifo cha TB Joshua kinamaanisha ushindi. Alikuwa feki, aliharibu maisha ya maelfu na alikuwa mchawi mkuu Afrika,”alisema.
TB Joshua, aliaga dunia Jumamosi akiwa na miaka 57.