Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amefutiwa kesi ya jinai katika mahakama ya wilaya na kufunguliwa upya katika mahakama ya mkoa.
Wakili wa serikali mkuu, Tumaini Kweka aliieleza mahakama hiyo kuwa licha ya kesi kupangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa na upande wa Jamhuri kupeleka mashahidi, Jamuhuri imeomba kuondoa shauri hilo katika mahakama hiyo ambapo sasa itasikilizwa katika mahakama ya mkoa.
Nafasi za Ajira Serikalini Bonyeza HAPANafasi za Scholarships Bonyeza HAPANafasi za Internships Bonyeza HAPA
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfulilizo siku ya Jumatatu tarehe 19/072021 katika mahakama ya Hakimu mkazi ngazi ya mkoa wakati kesi nyingine ya uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wawenzake itaendelea kusikillizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ngazi ya wilaya Julai 30, mwaka huu na watuhumiwa hao wamepelekwa gereza kuu la Kisongo kwa kuwa makosa yao hayana dhamana