Safari Luis Miquissone Yawadia, Akubali Dili la Al Ahly



IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Simba imepokea ofa mbili kutoka Ulaya kwa ajili ya Kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho raia wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone ‘Konde Boy’ mwenye umri wa miaka 26 ambapo bado klabu hiyo inajadili ofa hizo.

 

Hata hivyo, mwandishi wa habari za michezo wa Ghana, Nuhu Adams ameripoti kuwa nyota huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara amekubali kujiunga na Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri baada ya kukataa ofa ya kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

 

Taarifa kutoka Afrika Kusini zinadai ofa ya Kaizer Chiefs ya Shilingi Bilioni 1.6 imepigwa chini na Mnyama Simba huku Ahly wakiweka mezani kitita cha Tsh bilioni 2 kumnasa nyota huyo aliyejiunga Simba msimu wa akitokea UD Songo ya Msumbiji.

 

Iwapo atamalizana na Ahly, dau la Luis Miquissone litavunja rekodi kwa kuiingizia mkwanja Simba na kuwa usajili wa ghari zaidi kuwahi kufanyika kutoka Ligi Kuu Bara ukiacha lile la Emmanuel Okwi kutoka Simba kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia lililogharimu dola 300,000 (sawa na Tsh milioni 695.7) mwaka 2013.

.

Tetesi hizo zinasema kuwa, Rais wa Al Ahly amempigia simu Miquissone na kumweleza dhamira ya kumhitaji huku Kaizer Chiefs ikikata tamaa kumpata Luis kutokana na dau kuwa kubwa.

 

Al Ahly tayari wamefanya mazungumzo na Miquissone na kufikia makubaliano,Miquissone anavutiwa sana kucheza chini ya Pitso Mosimane ambae waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Mamelodi Sundowns.

 

Wakati dili la Miquissone kujiunga na Ahly likiwa limekamilika, tetesi zinasema kuwa Simba imefanya fasta kumvuta straika kutoka klabu hiyo Walter Bwalya waliyekuwa wakimwinda kwa muda mrefu. Aidha, kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na Timu ya Taifa ya Zambia, Clatous Chota Chama ameripotiwa kuwa ananyemelewa na Klabu ya Far Rabat ya Morocco.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad