Serikali Yasitisha Matamasha, Ibada za Mazishi Dakika 30




Serikali ya Tanzania imesitisha rasmi matamasha, sherehe na mikusanyiko na masharti kwa watakaolazimika kuwa na kibali maalumu kutoka kamati maalum ya Mkoa husika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi ameagiza idadi ya watu wanaokwenda kuwaona wagonjwa hospitali ipungue, waruhusiwe ndugu wawili tu asubuhi, na wengine wawili wataingia mchana au jioni. Hatua hiyo inalenga kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Wizara ya Afya imezuia mikusanyiko yote isiyokuwa ya lazima ikiwemo ya kidini na siasa, mpaka pale yatakapotolewa maelekezo mengine na endapo ikihitajika kufanyika mkusanyiko itabidi kitolewe kibali maalum

“Misiba yote ibada isizidi dakika 30 mpaka saa 1 na wahudhuriaji wawe wachache, hatujazuia kukaa misibani lakini mzingatie taratibu ikiwemo uvaaji Barakoa, unawaji mikono na kukaa umbali wa mita moja.


 
“Mahabusu wote wanaoingia gerezani kwa mara ya kwanza au Mtu aliyehukumiwa lazima apimwe kabla ya kuingia gerezani, lakini pia ndugu watakaokwenda kusalimia magerezani ataingia mmoja mmoja,” amesema Prof. Makubi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad