Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili leo imeanza kusikilizwa huku shahidi wa kwanza alieleza alivyokimbia kujificha Msikitini
Akitoa ushahidi katika kesi hiyo ya unyang’anyi wa kutumia silaha, shahidi ya kwanza, Mohamed Saad amesema alikimbilia Msikitini wa Kijenge baada ya Sabaya na wenzake kuingia dukani kwake na kumpa dakika tano afike dukani.
Shahidi huyo akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo alieleza Mahakama kuwa alikimbia kwa hofu kwani baada ya Sabaya kufika dukani kwake alipigiwa simu na ndugu yake Ally Saad kuwa Sabaya yupo dukani na amekuwa akiwasumbua wafanyabiashara.
Akiongozwa na wakili wa Serikali, Abdallah Chavula shahidi huyo amesema Februari 9, mwaka huu, Sabaya na wenzake walivamia dukani na kuchukua kiasi cha Sh 2,769,000 milioni.
Amesema baada ya Sabaya kuingia dukani na wenzake walijitambulisha kuwa ni maofisa wa Serikali ambapo walianza kumtafuta ndipo ndugu yake Noman Jasin alimpigia simu kuwa anatakiwa dukani.
Similar News:
Job Opportunity at Prime Minister’s Office, Procurement Officer
Alisema wakati anazungumza naye ndipo Sabaya alichukuwa simu na kumtaka ndani ya dakika tano afike dukani.
Alisema alikimbia kwenda kujificha Msikiti wa Kijenge na alikaa kuanzia saa 12 jioni hadi saa mbili na baadaye alikwenda kulala kwa rafiki yake eneo la Esso Makaburini.