Simba wafunguka sakata la Barbara na Manara



Baada ya Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Sunday Manara, kuweka hadharani chuki anazodaiwa kufanyiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa timu hiyo, Barbara Gonzalez, hatimaye uongozi wa Simba umetoa tamko.

Sauti iliyosambaa mitandaoni ambayo inadaiwa ni ya Manara, ilisikika ikisema:“Barbara una chuki mbaya sana kwangu hadi naogopa kula mbele yako, naacha hii timu kwa ajili yako kwa sababu ya chuki yako kwangu, unajiona wewe ni Simba kuliko wote, unataka umaarufu kinguvu.

“Unadhalilisha wafanyakazi wa Simba na kuwatishia, unatamani kuniondoa Simba, sitakubali na hujui lolote kuhusu hii klabu, subiri hii mechi ipite.

“Nasingiziwa eti nilienda Kigamboni kwenye kambi ya Yanga, vitu vya hovyo kabisa, mimi sinunuliki kwa thamani ya fedha Barbara kwangu haya ni matusi.”

Baada ya maneno hayo kuzuka, Championi lilimtafuta mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema: “Tunasubiri mechi ya Kigoma iishe ndipo tuweze kuongea nao na kutatua tatizo ila kwa sasa tumeweka akili zetu kwenye mchezo wa Kigoma.

“Suala la wao kwenda Kigoma au kutokwenda waulize wenyewe watakujibu.”

Jumapili hii Simba itakuwa ikicheza na Yanga kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho kule Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad