Soud Abdi Awaambia Yanga "Refa wa Pambano na Simba ni Yuleyule"



 
MWENYEKITI wa Kamati ya Waamuzi, Soud Abdi amesema Refa Ahmed Arajiga wa Manyara aliyeteuliwa kuchezesha fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baina ya watani wa jadi Simba na Yanga Jumapili Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma hatabadilishwa.
Abdi amesema amesikia malalamiko ya klabu ya Yanga dhidi ya refa huyo, lakini hawawezi kumbadilisha kwa sababu wakifanya hivyo hata Simba wanaweza kumkataa refa mpya.

Abdi ameomba Yanga wampe ushirikiano refa huyo hata akifanya makosa ya kibinadamu mchezoni, kwani makosa hutokea na ndiyo maana hata Ulaya wanatumia VAR.

Yanga iliishauri TFF kutafakari uamuzi wa kumteua Arajiga ambaye ametoka kuchezesha mechi mbili zilizopita za mashindano haya za watani wao, Robo Fainali na Nusu Fainali wakizitoa Dodoma Jiji FC na Kagera Sugar.  


Katika Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Arajiga atasaidiwa na washika vibendera Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono wa Tanga.
Arajiga aliingilia lawamani baada ya mchezo wa Nusu Fainali kwa kukubali bao pekee la Simba walilofunga kwa mpira wa adhabu waliouanzisha na kwenda kufunga wakati yeye anazungumza na wachezaji wa Azam FC.

Na ni tukio hilo limewafanya Yanga wapoteze imani mapema juu ya refa huyo pamoja na utetezi wa bosi wake, Abdi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad