Sports Countdown. Manara alikataa milion 4, Simba



Stori sita (6) za michezo (Sports Countdown) leo asubuhi Julai 22, 2021. kwenye Supa Breakfast ya East Africa Radio kuanzia Saa 1:15 Asubuhi, ambapo kila stori inatokana na namba 1 mpaka 6. Na moja ya stori kubwa leo ni Haji manara alikataa mshahara wa million 4 Simba.

6. Ni misimu ya ligi mfululizo ambayo mshambuliaji Robert Lewandowski amefunga mabao zaidi ya 40 kwenye kila msimu kwenye michuano yote akiwa na kikosi cha Bayern Munich kuanzia msimu wa 2015-16 msimu ambao alifunga mabao 42, toka hapo hajawahi kufunga mabao chini ya 42 ikiwemo msimu uliopita wa 2020-21 alifunga mabao 48 kwenye michezo 40, na sasa inaripotiwa mpachika mabao huyo raia wa Poland amevutiwa na ofa ya usajili aliyopewa na klabu ya Chelsea.


Ripoti zinadai Chelsea imefanya mazungumzo na wakala wa Mshambuliaji huyo Pini Zahavi ilikujua kama wanaweza kumsajili mteja wake katika dirisha hili la usajili la majira ya Joto, Chelsea wameamishia nguvu kwa Lewandowski baada ya kukutana na ugumu wa kumsajili Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut HÃ¥land. Lewandowski mwenye umri wa miaka 32 amebakiza mkataba wa miaka miwili na Bayern Munich.


5. Ni muda wa mkataba unaotajwa kuwa beki Raphael Varane atasaini ndani ya klabu ya Manchester United baada ya klabu hiyo kufanya makubaliano binafsi na mchezaji huyo. Inaripotiwa kuwa Varane amefikia makubaliano binafsi na mashetani hao wekundu na kilichobaki sasa ni Klabu yake ya Real Madrid kufanya mazungumzo na Man United juu ya ada ya uhamisho ya mchezaji huyo.


Varane mwenye umri wa miaka 28 ambebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake na Madrid, inatajwa kuwa thamani yake sokoni ni Pauni Milion 50 kiwango kinachotajwa kuwa Man United wapo tayari kutoa lakini Madrid hawataki kumpoteza beki huyo kwa hofu yakuwapoteza wachezaji viongozi wa safu ya ulinzi wote kwa pamoja hii ni baada ya Sergio Ramos ambaye alikuwa akicheza na varane kwenye safu ya ulinzi kuondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu uliopita.


4. Ni kiwango cha fedha kiwango cha milioni kinachotajwa kuwa ndio mshahara ambao alipaswa kulipwa Msemaji wa Simba Haji Manara kwenye mkataba ambao unadaiwa alipewa na klabu hiyo lakini hakuusaini kutokana na mgongano wa kimaslai na makampuni mengine anayofanyanayo kazi kibiashara kupitia mitandao yake ya kijamii binafsi na ndio sababu yakutosaini mkataba wenye thamani ya milion 4 kwa mwezi.


hii ni kwa mujibu wa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya hiyo upande wa mwekezaji Zacharia Hans Poppe.


Ufafanuzi huu ni kufuatia Haji manara kusikika akisema kuwa amekuwa akifanya kazi bila mkataba na amekuwa akilipwa mshahara wa laki saba (7) kwa mwezi, Haji alisikika akisema hayo kwenye sauti ambayo inaaminika alijirekodi akijibu tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akituhumiwa na Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez ikiwemo kuihujumu timu hiyo hususani ukaribu wake na baadhi ya viongozi na wadau wa mahasimu wao klabu ya Yanga ambao watapambana nao kwenye mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup.


3. Ni Hat trick aliyofunga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Richardson kwenye mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani mchezo ambao Brazili imeshinda kwa mabao 4-2 kwenye mchezo wa kundi D michuano ya Olimpiki, Mshambuliaji huyo anayecheza katika klabu ya Everton ya England amekuwa mchezaji wa kwanza anayecheza kwenye ligi ya Englanda EPL kufunga Hat trick kwenye michuano ya Olimpiki.


Brazili ambao ndio mabingwa watetezi wa Olimpiki kwa upande wa mpira wa Miguu kwa wanaume wameanza vyema kutetea taji lao kwa kupata ushindi huo mkubwa. Ukitoa mabao hayo matatu ya Richardson bao jingine la Brazil limefungwa na Paulinho wakati yale ya ujerumani yame fungwa na Nadiem Amir na Ragnar Ache.


2. Ni michezo mfululizo ya Simba SC aliyochezesha mwamuzi Ahmed Arajiga kwenye michezo ya kombe la Azam Sports Federation Cup na mwamuzi huyo ndiye atakayechezesha mchezo wa Fainali ya michuano hiyo msimu huu Kati ya Simba dhidi ya Yanga, mwamuzi huyo ndie aliyechezesha mchezo wa robo fainali kati ya Simba dhidi ya Dodoma jiji mchezo ambao Simba ilishinda kwa mabao 3-0, mchezo uliofata ni wa nusu fainali dhidi ya Azam na Simba walishinda bao 1-0 na sasa Julai 25, 2021 atakuwa akihusika kwenye mchezo wa 3 mfululizo unaoihusisha Simba.


Kutokana na mwamuzi huyo kuhusika kwenye michezo miwili mfululizo iliyoihusisha Simba kwenye michuano hii, klabu ya Yanga imesema umeshtushwa na TFF na Menejimenti ya mashindano hayo kumtumia mwamuzi huyo ambaye amehusika kwenye michezo mfululizo ya wapinzani wao kwenye mshindano haya na wanaamini kuna waamuzi wengi wenye uwezo hivyo kumrejesha mwamuzi mmoja kwenye mechi tatu (3) za timu moja katika shindano moja kinatia mashaka kwa uongozi wa klabu hiyo na mashabiki .


Na wameliomba shirikisho la mpira wa miguu kujitafakari juu ya matumizi ya mwamuzi huyo kwenye mchezo huu mkubwa wa Finali.


1. Ni medali pekee ya Gold aliyoshinda mcheza tennis namba moja Dunian Novak Djokovic kwenye michezo ya Olympic, alishinda medali hiyo mwaka 2008 kwenye michuano ambayo ilifanyika Beijing China, Djokovic raia wa Serbia ambaye ni mshindi wa mataji makubwa ya Tennis yani Grandslams mara 20 anapewa kipaumbela kushinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olympic 2020 ambayo pazia lake rasmi linafunguliwa leo.


Na kuelekea kwenye michuano hiyo mcheza tennis namba 5 Duniani mjerumani Alexander Zverev amejinasibu kuwa yupo tayari kumzuia Novak na amejipanga kuhakikisha anaibuka mshindi huku akisisitiza kuwa ili umfunge Djokovic unapaswa kucheza vizuri zaidi yake na kuhakikisha unautawala mchezo kwa kiwango kikubwa na anaamini haitakuwa rahisi kwa mserbia huyo kutwa ubingwa upande wa wanaume.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad