Takriban watu 125 wameripotiwa kufariki kutokana na ajali zinazohusiana na mvua kubwa ya masika iliyonyesha katika jimbo la magharibi la Mahastara nchini India.
Katika taarifa kwa waandishi wa habari serikali ya Mahasatara imesema kuwa mvua hio imesababisha maporomoko ya matope, mafuriko na kuporomoka kwa jengo.
Kupitia mtandao wa twitter Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesema amehuzunishwa na tukio hilo na kuahidi kuwa walioathirika watapewa usaidizi na serikali.
Waokoaji wanajitahidi kufukua vifusi vya tope kufikia nyumba zilizofunikwa na maporomoko ya ardhi. Karibu watu laki 9 wameokolewa kutoka maeneo yaliyoathirika na mafuriko.