Tokyo 2020: Mwamuzi wa kwanza wa kike kuvaa hijab katika historia ya Olimpiki



Sara Gamal ana rekodi ya kufikia mambo makubwa, na sasa mhandisi ,raia wa Misri na mchezaji wa mpira wa kikapu aliyegeuka kuwa mwamuzi yuko mbioni kutengeneza historia ya Olimpiki.

Atakuwa mwanamke wa kwanza wa Kiislamu aliyevaa hijab kuchezesha mpira wa kikapu kwenye michezo hiyo.

Sio hivyo tu, lakini aina ya mpira wa kikapu ambao yeye atakuwa mwamuzi mwezi Julai ni wa kwanza huko Tokyo.

Mpira wa kikapu wa 3x3 unafikiriwa kuwa mchezo unaochezwa zaidi ulimwenguni, maeneo ya mijini ambao umekua mchezo uliochezwa ulimwenguni kote katika mbuga na maeneo ya burudani, Ukijulikana kama mpira wa mtaani (Streetball) au Blacktop.

Inakadiriwa kuwa nchi 182 na zaidi ya wachezaji 430,000 ulimwenguni hucheza 3x3.

Sara pia atakuwa mwanamke wa kwanza wa Kiarabu na Mwafrika kuongoza mpira wa kikapu wa 3x3 kwenye Olimpiki.



Sara anasema kwensa kwenye Olimpiki ni ''ndoto''.
Janga la corona lilifanya kutokuwa na uhakika wa kuwepo kwa michezo hiyo

''Tulikuwa na wasiwasi sana kama itafanyika au la lakini hatimaye itafanyika.''

Familia yake yote imejivunia, alisema Sara. Lakini anafahamu kuwa kwa mafanikio hayo makubwa yanakuja na matarajio makubwa.

''Ni jukumu kubwa unapowawakilisha si tu wewe mwenyewe, lakini pia Afrika na ulimwengu wa Kiarabu. Si rahisi, lakini ninataka kuwa mwakilishi wao mzuri, hivyo ninaweka jitihada''.

Sara ni mpole anapozungumza, akionesha tabasamu la kirafiki. Anazungumza na mimi saa chache tu baada ya kuwasili nyumbani Misri akitoka kusimamia mechi ya mpira wa kikapu huko Romania.

'' Kila mara ninapofikia mafanikio na kuona kama ni jambo kubwa, Mwenyezi Mungu hunishangaza na kufungua fursa mpya ambayo huwa kubwa sana kuliko ya awali,'' ananieleza.

''Msimu uliopita niliteuliwa kusimamia mchezo wa nusu fainali ya ligi ya Misri ya wanaume. Hilo lenyewe ni mafanikio.''

Msimu huu Sara alichezesha fainali za kombe la Misri na ligi ya Afrika ya mpira wa kikapu kwa wanaume.

Hizo zilikuwa hatua kubwa kwangu, na waamuzi wengine wa kike nchini Misri, kwasababu ilikuwa mara ya kwanza kwa mwamuzi wa kike kuchezesha fainali ya wanaume nchini humo.''


Pamoja na mafanikio ya Sara ya hivi karibuni, safari yake kuelekea Olimpiki imekuwa ndefu.

Ilianza kama binti mdogo, aliyekuwa akimuangalia dada yake nkubwa akicheza mpira wa kikapu na kuongozana naye katika nyakati za mazoezi. Akiwa na miaka mitano, Sara alianza kucheza, na alipofika miaka 15 alikuwa mwamuzi.

Kwa miaka minane Sara alikuwa mchezaji na mwamuzi. Anasema kuamua kuacha kucheza na kujikita kwenye uamuzi ilikuwa moja kati ya changamoto kubwa.

''Si rahisi ukiwa wa kwanza kwenye hili-lazima uwe mwerevu kulitekeleza.

''Lakini ukiamini kwenye jambo fulani, lazima uamini kuwa utafanikiwa''.

Sara kufanya majukumu mengi mara moja. Bado anafanya kazi kama mhandisi, na alisoma kwa miaka mitano wakati akifuata ndoto zake za mpira wa kikapu.

Ilikuwa ni changamoto, anasema, "lakini nilikuwa na msaada wa familia yangu ambayo ilinifundisha kugawa muda wangu kati ya njia mbili"

Sasa wafanyakazi wenzake ni miongoni mwa wale wanaomshangilia.

"Wanaangalia michezo yangu na kwa kweli watakuwa wakinisaidia kwenye Olimpiki."

Ni imani hiyo hiyo inayoongoza anachovaa akiwa mchezoni. Sara ndiye mwamuzi wa kwanza wa FIBA kuvaa hijab katika kiwango cha kimataifa, kufuatia mabadiliko ya sheria mnamo 2017.

Sara anasema, anapokelewa vizuri kabisa.

"Wachezaji wengine hata wanasema mavazi yangu ni mazuri," anasema. "Ni vizuri kwangu kwamba nimefungua njia kwa waamuzi zaidi wa kike kuwa waaminifu kwa imani na ndoto zao."

Anasema waamuzi wanawake wachanga katika nchi yake mara nyingi humwandikia, wakisema kwamba walidhani "hawakuwa na nafasi ya kuwa katika mashindano makubwa au kusafiri ulimwenguni kote".

"Ninawaambia unaweza kufanya vizuri zaidi yangu. Unaweza kufikia malengo yako popote unapotaka. Una nguvu ya kuifanya.

"Ni heshima kubwa kuwa wanaweza kufikiria juu ya maisha yao ya baadaye kama waamuzi na kuona kwamba ikiwa watafanya kazi kwa bidii watatimiza ndoto zao."

Hicho ndicho anachokitaka kwa wasichana wadogo wa Kiislamu wanaomtazama kote ulimwenguni kujifunza kutokana na mafanikio yake, wakati wakimshuhudia uwanjani huko Tokyo.

"Weka umakini wako juu ya kuwa bora na weka lengo lako juu, basi unaweza kufika juu zaidi. Ninaamini kwamba sisi wanawake tuna nguvu za ajabu. Tuna nguvu sana."


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad