Tozo Mpya Miamala Ya Simu Gumzo





Julai 15, mwaka huu ndipo tozo mpya za miamala ya simu zitakapoanza kutumika ambapo ishu hiyo imekuwa gumzo.

 

Hivi karibuni, Bunge lilipitisha tozo ya kuanzia shilingi 10 hadi shilingi 10,000 kutozwa katika kila muamala wa kutuma au kupokea pesa na kiwango cha shilingi 10 hadi 200 kwa siku pale mteja atakapoongeza salio la muda wa maongezi kwenye simu ambapo kwa pamoja, Serikali inatarajia kukusanya wastani wa shilingi trilioni1.7 kwa mwaka.

 

Kuanza kwa tozo hizo ni utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/2022 ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alitoa siku 14 hadi Julai 15, mwaka huu kwa watoa huduma wote wa mitandao ya simu kurekebisha mifumo yao na kuanza kutoza tozo hizo mpya.

 

Hata hivyo, mjadala umejikita kwenye ongezeko la tozo hizo ambapo wengi wanatolea mfano wa endapo mtu anatuma au kutoa kiasi cha shilingi milioni 1, basi jumla ya gharama ya makato ni shilingi 31,800 kwa maana ya kwamba, gharama ya kutuma shilingi milioni 1 kwa wakala ni shilingi 14,900 na gharama ya kutoa shilingi milioni 1 ni shilingi 16,900.

Awali gharama zote za kufanya muamala wa shilingi milioni 1 ilikuwa ni shilingi 14,000 pekee, lakini sasa zimepanda maradufu.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wabunge wetu wanatakiwa kukatwa zaidi kulingana na kipato chao kisichokatwa hata kodi. Hii itawaumiza wananchi wa kawaida.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad