Trump afungua kesi dhidi ya kampuni za Twitter, Facebook na Google



Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amefungua mashtaka dhidi ya kampuni za Twitter, Facebook na You Tube.Trump mwenye umri wa miaka 75, amefungua mashtaka dhidi ya kampuni hizo za mitandao akitaka akaunti zake zilizofungwa, zifunguliwe mara moja.

Katika kesi iliyofunguliwa mjini Florida, Trump amezituhumu Facebook, Twitter na YouTube pamoja na wamilki wa kampuni hizo kwa kukiuka uhuru wake wa kujielezea.

 Rais huyo wa zamani wa Marekani aliyekuwa na wafuasi wapatao milioni 80 kwenye Twiiter, pia anataka kufungua kesi nyengine  kuwashirika watu wote waliofungiwa akaunti zao za kijamii baada ya Juni 1, mwaka 2018.

 Facebook na Twitter zilizifunga akaunti za Trump mnamo mwezi Januari muda mfupi kabla ya mwisho wa kipindi chake cha Urais. Kampuni hizo zilichukua uamuzi wa kuzifunga akaunti za Trump kwa kile kilichoelezwa kuwa alichapisha maneno ya kuchochea vurugu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad