Wizara ya afya ya Ukraine inachunguza kifo cha mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 47 ambae amefariki dunia muda mfupi jana jioni baada ya kupata chanjo virusi vya corona aina ya Pfizer.
Wizara hiyo imesema kunaweza kusiwepo na uhusiano kati ya hayo mawili na kwamba kulikuwa na watu wengine watano ambao walipata chanjo kutoka katika chupa iliyotumika kumchanja mtu huyo ambao wapo katika hali ya kuridhisha.
Kampuni ya Pfizer haikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia kitisho hicho. Hadi sasa zaidi ya watu milioni mbili wa Ukraine yenye jumla ya watu milioni 41, wamepata chanjo tangu Februrari.
Lakini hakuna kifo hata kimoja ambacho kimeripotiwa kutokana na chanjo hizo.