George Bush asema kuondolewa majeshi Afghanistan ni "makosa"




Rais wa zamani wa Marekano George Bush leo amekosoa hatua ya kuondolewa kwa vikosi vya majeshi ya muungano wa NATO Afghanistan akisema raia wanawachwa wakiwa "wanachinjwa" na wanamgambo wa Taliban.
Akizungumza na Deutsche Welle, Bush amesema ni jambo linalomvunja moyo kwasababu wanawake na wasichana wa Afghanistan watataabika pakubwa chini ya Taliban. 

Rais huyo wa zamani aliyekuwa chama cha Republican na ambaye alituma vikosi Afghanistan katika msimu wa mapukutiko wa 2001 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 huko New York, amesema anaamini Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anahisi vivyo hivyo kuhusiana na suala hilo.

 Bush amesema Merkel ambaye atastaafu kutoka kwenye siasa baadae mwaka huu baada ya miaka 16 madarakani, ameleta heshima kubwa katika nafasi hiyo ya Kansela na kwamba alifanya maamuzi magumu.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Picha uliyoweka hapo juu ya George Bush sio ya kweli huyo ni marehemu aliyesema na mtoto wake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad