Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekosolewa na raia wa nchi hiyo kwa kuzindua miradi wakati wa saa za amri ya kutotoka nje usiku.
Rais Kenyatta amezindua hospitali tano usiku wa Jumanne na kueleza kuwa ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo usiku ili kuhakikisha ufanisi katika utoaji wa huduma.
Alisema kuwa hospitali katika jiji mji mkuu, Nairobi, zinapaswa kufanya kazi saa 24 na alihitaji kufuatilia hilo.
Rais pia amesefafnua kuwa uzinduzi wa mchana ungekiuka miongozo ya watu kukaa mbali.
“Kama mlivyojionea wenyewe, haingewezekana kwenda na kufanya kile tulichofanya leo, wakati wa mchana kwasababu ya idadi ya watu ambao wangekuwa pale ,” aliwaambia wandishi wa habari.
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamemshutumu Bw Kenyatta kwa kutoheshimu sheria zake mwenyewe
“Kwanini Uhuru Kenyatta anafungua miradi usiku! Kwanini anakiuka amri ya kutotoka nje usiku? Haheshimu sheria zake mwenyewe pia, mbali na amri za mahakama ,” Ongoma alituma ujumbe wa twitter.
Rais Kenyatta anapaswa kesho kupelekwa katika mahakama ya sheria kwa kuvunja sheria ya saa za kutotoka nje usiku,” Miqdad Abdissalam aliandika..
“Sasa Uhuru anapaswa kuondoa amri ya kutotoka nje usikukwani pia yeye anaona umuhimu wa kufanya kazi saa za ziada usiku,” Ahmad Salim alituma ujumbe wa twitter.
Kenyatta
Amri ya kutotoka nje usiku nchini Kenya imewekwa kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri katika mji mkuu Nairobi na baadhi ya maeneo ya nchi inaanza saa moja jioni.