Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewaonya wenye tabia za kuwasajilia laini Watu wengine kwa kutumia Vitambulisho vyao vya Taifa (NIDA), endapo wakikopa na kushindwa kulipa watadaiwa wamiliki wa vitambulisho hivyo
Pia, Josephine Temu ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Biashara kutoka Kampuni ya Dun & Bradstreet inayokusanya taarifa za wakopaji amesema kwasasa Usajili wa Laini ya Simu humtaka mmiliki kuwa na Kitambulisho cha Taifa lakini baadhi ya Watu huwasajilia wengine bila kufahamu athari zake
Ameongeza “Kwa mikopo ya Simu, unapomsajilia mwenzio namba yake ya Simu anaweza kukopa akakimbia na ikaja kukupa shida wewe kwasababu umemsajilia kwa taarifa zako".