Wanne wakamatwa Uganda kwa tuhuma za kumshambulia kwa risasi Waziri





Polisi nchini Uganda imewawakamata watu wanne wanaoshukiwa kuhusika kwenye tukio la kushambuliwa kwa Waziri wa Kazi na Uchukuzi nchini humo, Katumba Wamala.
Mmoja wa washukiwa aliuawa wakati alipokuwa anakataa kutiwa nguvuni na Polisi.

Polisi wanasema washukiwa hao walipata mafunzo kwenye kambi moja na waasi wanaoendesha shughuli zao katika nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa Polisi, kundi hilo la washukiwa walipanga kufufua upya shughuli za kigaidi nchini Uganda.

Wakati wanatiwa nguvuni na Polisi, walikutwa na vifaa na mashine vinavyodhaniwa kutumika kwenye tukio la kushambuliwa kwa Waziri huyo, ambavyo vyote vimekamatwa.

Binti wa Waziri huyo na dereva waliuawa kwenye eneo tukio hilo lililofanywa na watu waliokuwa na boda boda wiki hii.

Rais Yoweri Museveni alizitaka mamlaka za ulinzi nchini humo, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu shambulio hilo na kuwafikisha wote waliohusika kwenye mikono ya sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad