Kwa mara ya kwanza hukumu ya kifungo cha gerezani imetolewa kwa mtu aliyehusika na uvamizi wa jengo la bunge na umwagaji damu mnamo Januari 6 katika nchi ya Marekani.
Paul Hodgkins mwenye umri wa miaka 38, alisema kuwa alijutia hatua hiyo kortini, ambapo alishtakiwa kwa "kuvamia jengo la bunge na kuzuia utendaji kazi wa wabunge".
Mwendesha Mashtaka wa serikali Randolph Moss alibaini kuwa Hodgkins alifanya shambulizi kubwa kwa demokrasia, lakini kwa sababu alikiri kosa, alipunguziwa hukumu ya kifungo cha miezi 18 gerezani kilichopendekezwa na waendesha mashtaka.
Hodgkins alihukumiwa kifungo cha miezi 8 gerezani na mahakama.
Ilielezwa kuwa hukumu iliyotolewa kwa Hodgkins Florida inaweza kuwa kielelezo kwa takriban wafuasi 230 wa (Rais wa Zamani wa Marekani Donald) Trump ambao walizuiliwa kwa sababu ya uvamizi wa bunge mnamo Januari 6 na wanasubiri kuhukumiwa kwa shtaka moja.