Polisi Hong Kong leo wamemkamata mhariri wa zamani wa gazeti la kutetea demokrasia la Apple Daily. Lam Man-Chung amekamatwa wiki chache baada ya gazeti hilo kulazimika kusitisha shughuli zake, baada ya maafisa kuzuia mali zake zenye thamani ya dola milioni 2.3.
Gazeti la South China Morning Post limesema kuwa Lam aliyekuwa mhariri mkuu wa Apple Daily amekamatwa kwa tuhuma za kula njama ya kushirikiana na watu kutoka nje kuhatarisha usalama wa taifa.
Lam, mwenye umri wa miaka 51 ni mtu wa nane aliyekuwa anafanya kazi na gazeti la Apple Daily ambao wamekamatwa katika wiki za hivi karibuni. Mwezi Juni, polisi ilizivamia ofisi za gazeti la Apple Daily na kuchukua vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta kama ushahidi