Al-Shabab wa Somali wapongeza Taliban kwa kuteka Afghanistan





Vyombo vya habari vinavyojihusisha na kundi la wanamgambo wa Kiislamu lenye makao yake nchini Somalia al-Shabab vimefurahia kuanguka kwa serikali inayotambuliwa kimataifa ya Afghanistan na kupongeza Taliban kwa kuuteka nchi hiyo.
"Mungu ni mkubwa: mji wa Kabul unaangukia kwa majeshi ya Imarati ya Kiislamu", tovuti zinazounga mkono kundi la al-Shabab Calamada na Somali Memo zimeandika katika vichwa vya habari vilivyofanana.

"Sherehe zilianza kote nchini, huku bendera inayoashiria kuabudu Mungu mmoja ikipandishwa katika viwanja vikuu vya Kabul na picha zilizotolewa na Imarati wa Kiislamu zikionyesha mujahideen wakishika doria katika vitongoji vilivyo karibu na Kabul wakati maisha yanarejea katika hali ya kawaida", Calamada.com imeripoti.

Ripoti hiyo imesema kuwa Taliban wameshinda viongozi vibaraka wa "Afghanistan" na "mamia ya maelfu ya wanajeshi wa kigeni" baada ya miaka 20 ya kupigania jihadi.

Al-Shabab ina uhusiano na al-Qaeda na imekuwa ikipiga vita vikosi vya Somali vyenye kuungwa mkono na Umoja wa Afrika tangu katikati ya miaka ya 2000.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad