Aliyesimamishwa kazi akidaiwa kuigiza kuchanja Covid-19 afunguka




Arusha. Mkuu wa idara elimu msingi  halmashauri ya Jiji la Arusha, Omary Kwesiga amesema ameshangazwa kusimamishwa kazi akidaiwa kufanya igizo la kuchomwa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 .

Amesema picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa hakuchomwa chanjo hiyo zimechezewa, na  kubainisha kuwa alichanjwa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Agosti 6, 2021 Kwesiga amesema anashangazwa na video hiyo, "nimezuiwa kuongea na vyombo vya habari kulingana na maadili ya kazi na kikubwa mimi nimechanjwa nina ushahidi na nipo Salama."

Ofisa huyo na ofisa muuguzi msaidizi  wa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru,  Scolastica Kanje leo wamesimamishwa kazi na mamlaka zao kwa tuhuma za kufanya igizo la kuchanja.


 
Kwa takribani siku tatu  video hiyo inayomuonyesha  Kwesiga na Kanje wakifanya kile ambacho kimetafsiriwa ni maigizo imebua mjadala mitandaoni

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad