Amber Rutty Yamkuta Tena, Achezea Kipigo cha Mbwa Koko




MSANII Rutyfiya Abubakary ‘Amber Rutty’ yamemkuta mazito tena baada ya kutembezea kichapo na mumewe Said Bakary. Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyu kujikuta kwenye matatizo kutokana na ugomvi wa mara kwa mara na mumewe huyo ambaye waliwahi kutiwa gerezani kwa msala wa picha za utupu.

Mapema leo, Amber ameposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa amechoshwa na vipigo vya mara kwa mara anavyovipata kutoka kwa mumewe huyo.

Kwenye video hiyo, Amber ameonekana akivuja damu puani huku mumewe akisikika akigonga mlango lakini yeye akikataa kumfungulia kwa kudai hajafanya kosa lolote.

Baadaye, mrembo huyo aliposti mawasiliano yake ya ujumbe mfupi na kuonesha aliyemponza hadi kupokea kichapo hicho ni msanii wa Bongo Fleva, Enock Bella wakati ameshamuambia hamtaki lakini yeye bado anamng’ang’ania.

Akaenda mbele zaidi kwa kuposti sauti aliyodai ni ya Bella alipokuwa akimtongoza. @hotpot_tz ilijaribu kumtafuta Bella simu yake haikuwa hewani. Alipotafutwa mume wa Amber alikiri kumdunda mkewe huyo kutokana na hasira alizokuwa nazo.

‘‘Ni kweli nilimpiga kidogo sababu ya hasira. Aliniudhi kwani amekuwa akiwasiliana na mwanaume mara kwa mara hadi usiku,’’ alisema Said. Alipoulizwa mwanaume huyo ni Bella, alikiri kuwa ndiye.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad